Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael, maarufu Lulu, amebadilishiwa adhabu na sasa anatumikia 'kifungo cha nje' kwa amri ya Mahakama Kuu Tanzania.
Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.
Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tananzia, Dar es salaam.
"Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje, kitaalamu tunaita ' Community service'' amesema Mboje
Post a Comment