Ramadhan ndugu yenu, nimekuja toka mbali, Nimetoka kwa Mola wenu, Muweza Mola Jalali.
Kanipa salamu zenu, na zawadi mbali mbali, Mnipokee niwe kwenu, Ndugu zangu tafadhali,
Mimi ni wenu mgeni, kunifukuza muhali, Kwa mwaka nakujieni mara moja hilo kweli,
Mwezi mmoja oneni, si miezi kumi na mbili, Sikai ndefu zamani, kwa hali zenu kujali,
Mekuja kwa maandishi, ujio wangu halali, Nilobeba siregeshi, kwa watakao nikubali.
Kusanyeni hayaishi, jamani nasema kweli, Pia nnayo marashi naosha roho pia mwili,
Nimefikisha saum nayo ni nguzo kamili, Kama mutanikirimu, Mola atawafadhili.
Nafsi atazikimu, zistawi zenu hali, Lengo mumche Alimu, ni yake hii amali.
Jina langu Ramadhani, Ziara yangu neema, Waislamu fungeni, Mpate afya njema
Jina langu Ramadhan, ziara yangu neema, Waislamu fungeni, Mpate afya njema........
Post a Comment