MTAANI dot com ni jina la audio ya wimbo mpya aliowahi kuachia Kenyan rapper Colonel Mustafa akishirikiana na mwanadada Avril ambaye amefanya chorus. Ngoma ilitoka mwaka 2009 na ilitayarishwa na Ogopa Deejays pamoja na video yake. Kupitia Mtaani dot com jamaa amezungumzia maisha halisi ya mtaani jinsi watu wanavyofanya harakati zao za kila siku katika kutafuta mafanikio na kutoka kimaisha. Ni wimbo mzuri wenye mashairi yanayogusa na yanayoweza kuishi zaidi sababu bado yanaendelea kutokea kila siku. Usichokifahamu kutoka kwa mustafa ni kwamba baba yake ni Mkenya na mama yake ni Mtanzania. Ok nakukaribisha kusikiliza/ download kisha share na wana muziki mzuri. Enjoy.
Post a Comment