Bablee ku-perfom Morogoro siku ya Sabasaba
STAR wa muziki wa Bongo Flava Tanzania anayetamba na ngoma yake mpya True Story Bablee, anatarajia kukiwasha pande za Morogoro kwenye event ya Miss bwawani itakayofanyika siku ya tarehe 7 julai (saba saba) mwaka huu. Akiongea na Bongo Exclusive mwanamuziki huyo amesema kuwa watu watarajie suprises za kutosha kutoka kwake kwani siku hiyo hatakuwa peke yake atasindikizwa na Cobra singeli, Miss kisura (Diana Ibrahim) na wengine wengi. Show hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa Le Grand View Motel kuanzia saa moja jioni kwa kiingilio cha shilingi 5000, Planet ndiye atakaye-host siku hiyo. Imetayarishwa na Planet Project Fame pamoja na Sayari TV. Bablee ni mmoja kati ya wasanii wakubwa nchini Tanzania walioweza kuikuza game ya muziki wa Bongo Flava na kuweza kufanya vizuri Africa mashariki na kwengineko duniani kwa miaka 17 sasa. Baadhi ya ngoma zilizomtambulisha vyema zaidi ni pamoja na Kizizi, Chagua Moja, Mapenzi Vionjo (Aliyomshirikisha mwanadada Queen Darleen), Dhamira, Majukumu na nyengine nyingi. Kwa habari zaidi unaweza kuLIKE page yake hapa.