Mahitaji
- Nyama ya ngombe 1/2 kilo
- Vitunguu maji viwili
- Nyanya nne
- Pilipili hoho nusu
- Kabichi 1
- Viazi vinne
- Karroti 1
- Njegere nusu kikombe
- Mafuta vijiko vitatu vya supu
- Kitunguu saumu
- Pilipili manga kiasi
- Kata nyama,osha,weka chumvi,kitunguu saumu na pilipili manga acha chemsha na uikoroge ili viungo vikolee,ongeza maji kuifunika nyama,acha iive
- Kata kabichi kama vile unavyokata la kachumbari lioshe na maji ya vuguvugu,Tayarisha kitunguu,nyanya,karoti,viazi vigawe mara mbili.
- Injika chungu jikoni,weka mafuta yapate moto,kaanga kitunguu mpaka kibadilike rangi kiwe hudhurungi,weka nyanya,viazi,supu ya nyama na nyama uloichemsha,acha nyanya iive mpaka ipondeke.Na mchuzi uwe mzito.
- Weka carrot na njegere pamoja na kabichi.Acha viendelee kuiva sosi ya kwenye kabichi ikikaribia kukauka weka pilipili hoho acha vichemke dakika kadhaa kisha epua.
- Ongezea chumvi ikiwa haijatosheleza