Tabia hizi akiwa nazo mwanaume husababisha ndoa au mahusiano kudumu
Katika zama hizi kutafuta mwanaume sahihi wa kuwa nae kwenye mahusiano imekuwa ngumu kama ilivyo kwa ngamia kupita katika tundu la sindano hasa katika kizazi hiki cha kisasa. Kuna mambo machache ambayo mwanaume akiwa anayafanya kwa mwanamke wake kunaweza kumfanya awe mwanaume sahihi kwa wakati huo; hii ikiwa na maana kwamba hata mwanamke akiambiwa habari za kufunga pingu za maisha na mwanaume huyu hatakuwa na sababu ya kubisha.
Hapa chini tumekukusanyia orodha ya tabia ambazo wanawake wengi wanasema kwamba, mwanaume akiwa nazo basi mwanamke hatasita kuwa nae kwenye mahusiano:
1. Matendo yake ni sawa na anachokiongea
Mwanaume anaweza akakuambia anakupenda asubuhi mpaka jioni. Akakwambia maneno yote matamu unayotaka kusikia, lakini swali Je? Ni kweli anakupenda? Lazima uangalie matendo yake, kwa maana matendo pekee ndio yatakufanya uamini asilimia zote kama kweli anakupenda, na kama unaona matendo na maneno yasemwayo yako sawa basi mwanaume huyo ni wako.
2. Huangalia mapungufu yako na kuyaona si kikwazo
Mwanamke anapotafuta mwanaume sahihi si kwamba yeye ni sahihi, hapana, kila mtu duniani hapa aliumbwa na mapungufu yake. Unapopata mwanaume ambaye anafahamu mapungufu yako na hayachukulii kwamba si kikwazo kwa nyie kuwa pamoja na wala hakwaziki kila siku kwa sababu ya mapungufu yako, huyo ni mwanaume sahihi kwako.
3. Anayemfanya mwanamke ajisikie yuko katika mikono salama
Mwanamke kujisikia yuko salama, kunaweza kukawa kimwili, hisia ama imani. Kila mwanamke anahitaji kujisikia yu salama mikononi mwa mwanaume wake, ni mwanaume mwema pekee anaweza kujitoa katika hilo.
4. Mwenye kutoa msaada unaohitajika
Nini maana ya kuwa kwenye mapenzi kama hupati msaada wowote? Kama mahusiano hayo kwa namna moja au nyingine hayafanyi maisha yako yabebeke kwa unafuu? Kama ilivyo kwenye usalama, na msaada kwa mpenzi huwa unakuja katika njia tofauti tofauti. Mwanaume yeyote anayetoa msaada kwa mwanamke wake huwa ni mwanaume sahihi. Na ni kwa mwanamke mjinga na mpumbavu pekee atakayeona hili halifai.
5. Mwenye kuonyesha mamlaka juu ya mwanamke (Over-possessive)
Kuna wanaume wengine mwanamke akiamka asubuhi anajuta kusema ‘sawa’ wakati alipotongozwa. Mwanaume anataka ajue kila kitu anachofanya mwanamke wake na chochote kile anachopanga kufanya, na bila kusahau muda atakaotumia kufanya yote. Mwanaume anatakiwa aelewe tofauti kati ya kuwa na wivu kwa sababu fulani fulani na kuwa ‘a control freak’ au mwenye wivu wa kijinga.
6. Mwanaume anayedhani sio lazima awe kwenye ratiba ya mwanamke wake
Kuna wanaume wengine lazima wazue mjadala hata mwanamke atakapoamua kununua nguo yake ya ndani bila kumpa yeye taaarifa. Au akitaka kutoka na kufurahi na wenzie (Girls night out) lazima naye awepo (Kitu Bumper to bumper). Mwanaume sio kila ratiba ya mwanamke wake awemo, (It’s a turn-off when you are too available – I mean man, get a
life!!!).
7. Sio mlalamishi
Hamna kitu kinakera kama mtu anayelalamika kila wakati. Kwa kweli mwanaume anayelalamika kwenye kila anachokiona ni turn-off (anakera na kuchosha). Mwanaume hutakiwi kulalamika kwa vitu vidogo vidogo. Hata hivyo vikubwa vyenyewe unatakiwa useme mara moja, kwa sauti yako ya kiume lazima mwenza wako ataelewa na kujirekebisha.