Dully Sykes Feat. Sebastian Ndege | Leah (Audio)

featured imageDully Sykes Feat. Sebastian Ndege | Leah (Audio)

Dully Sykes Feat. Sebastian Ndege | Leah


LEAH alikuwa ni binti ambaye alibahatika kufika katika kipindi cha NJIA PANDA cha CLOUDS FM ambacho kiliongozwa na SEBASTIAN NDEGE.

Katika kipindi hicho LEAH alieleza changamoto zake za kimaisha ambazo ziliwagusa wasikilizaji wengi wa kipindi cha NJIA PANDA na wengi walijitokeza kumsaidia kwa kadri walivyoweza ikiwemo suala zima la matibabu yake.

LEAH akiwa katika tumaini jipya la kurudisha furaha yake iliyopotea mwenyezi Mungu nae akamuita mja wake. LEAH alifariki na kuzikwa katika makaburi ya Makuburu Tabata.

DULLY SYKES Baada ya tukio hilo ikabidi aingie studio na kuimba wimbo uliohusu maisha ya mwanadada LEAH kwa 100%.

Wimbo huu ulipotoka uliweza kuteka hisia za watu wengi sana na kumjengea Heshima pia DULLY SYKES katika Muziki wake.

MASHAIRI YA WIMBO WA LEAH

[Verse 1]

Nilimkuta Leah amejilaza/
Chini kwenye kituo cha wamataa/
Huku ngozi yake maji ya kunde Imegeuka ya manjano isiyopendeza/
Unafanya nini nikamuliza/
Akanijibu anaumwa na pia ana njaa/
Msichana wa miaka wa kumi na tisa/
Kumbe alikuwa amesha hadhirika/
Nikampeleka duka la madawa/
Hili kidonge kidogo vimweke sawa/
Kwani alikuwa na fungus mwili mzima/
Ikambidi anihadithie stori nzima/
Akaanza kuniadhithia kwa huruma/
Kwamba siku mmoja alikuwa anatoka shule Leah siku hiyo njaa ilimtawala/
Akatokea dereva wa daladala/
Akamwambia Leah lifti panda mbele/
Japo mwanafunzi akae kiti cha mbele/
Tena bila malipo ni burebure/
Akaanza kumtongoza polepole/
Sababu Leah njaa ilimtawala/
Akaambiwa atanunuliwa Chipsi Soda/
Ilipofika jioni akanunuliwa/
Wakapanga wakutane tena Palepale/
Ilipofika siku wakakutana pale/
Akapanda daladala hadi usiku/
Wakaenda kufanya yao mavitu/
Wakaenda kufanya yao mavitu/

[Chorus]

Leah Umekwenda
Hayo yote Mola amepanga 3x

[Verse 2]

Akamrubuni na kumfanya mapenzi/
Akawa akitoka shule yeye kwa mchizi/
Kwa bahati Leah shule alimaaliza/
Baada ya tu kumaliza akatoroshwa/
Akaishi naye kama mke na mume/
Nyumbani alikuwa na majukumu yote/
Kuosha vyombo kupika na khadhalika/
Ikawa akikosa kidogo anapigwa/
Baadae mwanaume akawa na kisirani/
Akawa anaingia Wanawake ndani/
Alivumilia mpaka mwisho kashika mimba/ Alikaa nayo mpaka miezi tisa/
Alijifungulia huko Muhimbili/
Mtoto akafa baada ya miezi miwili/
Alikufa kwa ugonjwa wa Nimonia/
Baadaye Leah naye aliuguwa/
Alikuwa na tatizo la kifua/
Tuberculosis ndiyo iliyomsumbuwa/
Muda wa wiki mbili alisumbuliwa/
Ilipofika Tarehe sita mwezi wa kumi/ Nakumbuka siku hiyo ilikuwa jumapili/
Ndipo siku hiyo Leah alifariki/
Ilipofika Jumanne tarehe nane/
Ikabidii watu wote tuungane/
Tukamzika Tabata Makuburi/
Hapo ndipo yalipokuwa makaburi/
Mungu mlaze mahali pema peponi x 2 Leah

[Chorus]

Leah Umekwenda
Hayo yote Mola amepanga 3x

[Outro]

Naitwa Sebastiani Ndege Mzee wa Njia Panda.
Jamii yetu haina budi kuwawezesha vijana kukabiliana na mazingira yanayowazunguka kwa kuwapa elimu bora ya afya ya uzazi, malezi bora kuanzia ngazi ya familia na hadi sheria na sera zinazomjenga kijana na jamii kwa ujumla.

Shukrani kwa wana njia panda kwa kujitolea misaada mbalimbali kwa Leah na hata kumsomesha.

Mungu ailaze roho ya marehemu Leah mahala pema peponi amina

[Chorus]

Leah Umekwenda
Hayo yote Mola amepanga 3x

DISCLAIMER:
No copyright infringement intended.
I do not own the audio in this video. They belong to their rightful owners.

https://www.youtubepp.com/watch?v=RwBXZ1tuBUw

Install Bongo Exclusive app from Google Playstore here https://play.google.com/store/apps/details?id=bongoexclusive.tv

Bongo Flava is the nickname for Tanzanian music. The genre developed in the 1990s, mainly as a derivative of American hip hop and traditional Tanzanian styles such as taarab and dansi, with additional influences from reggae, R&B, afrobeat, a combination that forms a unique style of music. Lyrics are usually in Swahili or English. – Source WIKIPEDIA


This Is Bongo Exclusive Official Website! For Latest Urban Music, Bongo Flava, Celebrity Gossips, Breaking News, Lifestyle, Fashion, TV Series. biography, album mp3, download

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post