Connect with us

Hi, what are you looking for?

News

Mangwair “a.k.a mimi” -The Album, Produced by P.Funk [Bongo Record].

a.k.aMimi 2

 Mangwair "a.k.a mimi" -The Album, Produced by P.Funk [Bongo Record].

“a.k.a mimi” – Name of the Album, Produced by P.Funk {Bongo Record}.

1. MIKASI
➡️ft Mchizi Mox, P.Funk, Rah P, Mkoloni & Ferous
 
➡️
Nyimbo ambayo inaelezea maisha ya ujana/vijana unapofika muda wa jioni.
Wengi wao hukutana na kupiga mahesabu ya kwenda kufanya starehe Clubs
na sehemu nyngn kwa kuchangishana. Pamoja na hayo dhamira kuu inakuwa ni
kwenda kutafuta wanawake hali ya kuwa wanawake wenyewe wanakuwa
wanajiuza.
➡️
Mashairi katika nyimbo hii yamewekwa katika mpangilio wa vina wenye
mtiririko mzuri na unaovutia zaidi bila kuharibu kile wanachokieleza kwa
kupokezana.

2. BADO NIMO
➡️ featuring T.I.D (before Mnyama)
➡️Hi ndio nyimbo ambayo jina la album limesikika saana “A.K.A MIMI” kiasi kwamba wengine wanaiita hii nyimbo a.k.a mimi.
 
➡️Mashairi
yamepangwa katika mtiriko mzuri kwa kuzzingatia vina bila kupoteza
ujumbe uliokusudiwa. Katika wimbo huu Ngwair amejikita zaidi kuelezea
kuhusu ugonjwa wa ukumu. Amesimama kama yeye ndio UKIMWI wenyewe ambapo
ametaja majina tofauti tofauti ambayo yanajulikana lakin pia ameelezea
namna gani Ukimwi unaambukizwa na ameeleza upo kwa wengi huku akiondoa
dhana ya kuwa viongozi wa dini hawawezi pata ukimwi.
➡️ Pia, ameeleza namna gani huu ugonjwa umekosa dawa japokuwa watu wngn wanaaminisha kuwa zipo dawa.

3. ZAWADI
➡️Hii
ni nyimbo nyingine ambayo Ngwair ameongelea suala zima la ugonjwa wa
UKIMWI. Tofauti na “Bado nimo”, humu Ngwair kaeleza zaidi namna gani
wanawake wanashawishika kwa vitu vidogo vidogo ambavyo ndio tunasema
Zawadi huku akielezea namna gani alikutana na binti akawa na mahusiano
nae na mwishoe kumuambukia UKIMWI
➡️
Katika nyimbo hii unamsikia Ngwair akimuoffer bint ataje zawadi yeyote
aitakayo huku bint akimjibu ya kuwa Zawadi ya HIV tayar imemtosha.
➡️ Kati ya nyimbo mzuri saaana yenye maelezo ya jinsi Ngwair anavyomhesabia bint zawadi alizompatia

4. DAKIKA MOJA
 
➡️Featuring Noorah (Baba Styles)
➡️
Hii nyimbo inaelezea kijana alivyokutana na bint katika moja ya kumbi
za starehe na kuvutiwa nae huku akimuomba japo dakika moja ya kuweza
kuongea nae, ndipo jina la nyimbo linapopatikana.
➡️
Hii ni moja ya nyimbo ambayo vijana wengi wa wakati nyimbo inatoka
walitumia saana mashairi ya huu wimbo kutongozea wanawake kwani ilikuwa
na maneno ya kusifia na kulainisha zaidi.

5. GHETO LANGU
➡️Achana
na Ghetto ya Akon, hii ni tofauti kidogo. Ni nyimbo iliyojawa na
majisifu kuhusu chumba (gheto). Katika nyimbo hii Ngwair amesifia saana
chumba chake huku akiorodhesha vitu mbalimbali ambavyo vipo ktk gheto
lake la Dodoma na lile la Kijitonyama.
➡️
Ngwair ameenda mbali kwa kuelezea namna marafiki zake wamekuwa wakienda
hapo gheto kwake na wanawake zao lakin mwisho wa siku wanawake wanafall
in love na Ngwair sababu ya Gheto

…. Kwa leo ngoja niishie hapo ila kwa wengine wanaweza endelea kuchambua;
 
6. Mademu Wangu
 

7. She got a Gwan
 

8. Weekend
 

9. Pokea simu
 

10. Sikiliza

Written By Hamza Athumani Mkata
Hamza Athumani Mkata

Advertisement. Scroll to continue reading.
Written By

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You May Also Like